Wanachama wa TUGHE Zaidi ya 800 wamefanya utalii wa ndani kwa kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro siku ya Alhamisi tarehe 18 Septemba 2025 kwa lengo la kuunga mkono juhudi za kukuza utalii wa ndani na kutambua fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii.
Katika ziara hiyo, wageni walipata nafasi ya kuona vivutio mbalimbali vikiwemo maporomoko ya maji, mimea ya kipekee na mandhari ya Mlima Kilimanjaro maarufu kama “Paa la Afrika”.
Katibu wa TUGHE, Hery Mkunda, alisema kuwa ziara hiyo imewapa uelewa mkubwa zaidi wa thamani na uzuri wa urithi wa dunia.
Naibu Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Steria Ndaga, aliwapongeza TUGHE kwa kuunga mkono utalii wa ndani, akibainisha kuwa kutembelea hifadhi kunasaidia kuongeza pato la taifa na ajira kwa vijana.
Naye Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi TANAPA, Jully Bede Lyimo, aliongeza kuwa utalii wa ndani una faida nyingi zikiwemo kuongeza mapato, kuchochea ajira, kukuza biashara ndogo ndogo na kujenga uzalendo wa taifa.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro, Amri Mtekanga, aliwakaribisha wageni hao na kuwaeleza vivutio pamoja na taratibu za kupanda Mlima Kilimanjaro.
Ziara hiyo ya TUGHE imedhihirisha mshikamano wa Watanzania katika kuunga mkono sekta ya utalii kuelekea maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani.
Shamrashamra wakati wa utalii huo wa ndani.
Utalii wa ndani ukifanyika.
Friday, September 19, 2025
WANACHAMA TUGHE WATEMBELEA HIFADHI YA MLIMA KILIMANJARO
Tags
# Habari
Kuhusu - Singidaniblog
Habari
Tags:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
𝗡𝗶 𝗰𝗵𝗼𝗺𝗯𝗼 𝗰𝗵𝗮 𝗵𝗮𝗯𝗮𝗿𝗶 𝗸𝗶𝗻𝗮𝗰𝗵𝗼𝘁𝗼𝗮 𝗵𝗮𝗯𝗮𝗿𝗶 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝘁𝘂𝗸𝗶𝗼 𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶 𝗻𝗰𝗵𝗶𝗻𝗶 𝗧𝗮𝗻𝘇𝗮𝗻𝗶𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝗼𝗸𝗼𝘁𝗲 𝗱𝘂𝗻𝗶𝗮𝗻𝗶 ,𝗸𝘄𝗮 𝗸𝘂𝗷𝗮𝗹𝗶 𝘄𝗲𝗹𝗲𝗱𝗶 𝗻𝗮 𝘁𝗮𝗮𝗹𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗵𝗮𝗯𝗮𝗿𝗶. 𝗞𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗔𝗡𝗚𝗔𝗭𝗢 𝗡𝗔 𝗛𝗨𝗗𝗨𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗛𝗔𝗕𝗔𝗥𝗜, 𝗪𝗔𝗦𝗜𝗟𝗜𝗔𝗡𝗔 𝗡𝗔𝗦𝗜, 𝟬𝟳𝟱𝟰 𝟯𝟲𝟮 𝟵𝟵𝟬. 𝟬𝟲𝟴𝟴 𝟵𝟭𝟰 𝟯𝟰𝟰 𝗘𝗺𝗮𝗶𝗹: 𝘀𝗶𝗻𝗴𝗶𝗱𝗮𝗻𝗶𝟳𝟳@𝗴𝗺𝗮𝗶𝗹.𝗰𝗼𝗺,












No comments:
Post a Comment