YANGA DAY KEMONDO WILAYA YA BUKOBA KAGERA YAADHIMISHWA KWA SHUGHULI ZA KIJAMII - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, September 13, 2025

YANGA DAY KEMONDO WILAYA YA BUKOBA KAGERA YAADHIMISHWA KWA SHUGHULI ZA KIJAMII

Afisa Tarafa ya Katerero iliyopo Bukoba mkoani Kagera Bwanku M Bwanku Jana Ijumaa tarehe 12/09/2025 ameungana na wanachama na mashabiki wa Timu ya Yanga Kata ya Kemondo kusherekea Kilele cha Siku yao Maarufu ya Mwananchi.

 Kama Mgeni rasmi. Shughuli ilianza kwa kufanya usafi Sokoni Kemondo, kutoa vyakula kwa wagonjwa, kuchangia damu chupa 50 na kupanda miti kwenye Hospitali ya Wilaya ya Bukoba- Bujunangoma na baadae kufanya sherehe kubwa na ya aina yake kwenye Ukumbi wa Kemondo Resort- Kemondo.

Bwanku aliwapongeza kwa kuanzisha Kikundi chao cha YANGA FAMILY kwa ajili ya kusaidiana kwenye shida na raha na kugusa jamii kwenye maeneo mbalimbali chini ya Mwenyekiti wao wa Yanga Kata ya Kemondo Bi. Levina Soteli.

Aidha, Bwanku alitumia sherehe hiyo kupitia hotuba yake kuwahimiza Wana Yanga hao kuendelea kulinda amani ya Taifa hasa kwa mwaka huu wa Uchaguzi na kutumia haki yao ya msingi kupiga kura ikifika siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025. 

"Niwapongeze Wana Yanga wa Kata yetu ya Kemondo kwa jambo hili kubwa, mimi Afisa Tarafa nawachangia pia kutunisha mfuko wenu lakini msisahau kutunza amani ya nchi yetu hasa mwaka huu wa uchaguzi

"Kwa sababu tumekutana hapa niwajuze pia masuala ya maendeleo yaliyopatikana Kata yetu ya Kemondo ndani ya kipindi cha Rais Samia Suluhu Hassan ikiwemo ujenzi wa Hospitali na Halmashauri ya Wilaya na upanuzi wa Bandari ya Kemondo.

Bandari yetu upanuzi wake umegharimu Sh.Bilioni 20, mradi mkubwa wa maji wa Bilioni 15.8 ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Kanazi B, taa za barabarani Kemondo na miradi  mingine mingi." alisema  Bwanku na kuwaeleza wana Simba kuendelea kulinda amani ili maendeleo yapatikane zaidi.

Klabu ya Yanga hufanya Tamasha hili kubwa la Wananchi kila mwaka ambapo wanachama na mashabiki wa Simba nao huungana nchi nzima kufanya matukio mbalimbali na Kilele cha Yanga Day mwaka huu kilikua leo kwenye uwanja wa Mkapa- Dar es Salaam ambapo wachezaji wapya wa shughuli walitambulishwa.

Matukio mbalimbali ya maadhimisho hayo.







Keki maalumu ya maadhimisho hayo ikikatwa.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad