NI WAKATI MWAFAKA KUANZISHA 'HUB YA KITAIFA' MTANDONI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, September 13, 2025

NI WAKATI MWAFAKA KUANZISHA 'HUB YA KITAIFA' MTANDONI

Mijadala kuhusu ajira za vijana ikifanyika

....................................

Na Godwin Myovela

Kadiri uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 unavyokaribia, mjadala kuhusu ajira za vijana umeongezeka. Kila mwaka, maelfu ya wahitimu wa VETA, vyuo vikuu na vyuo vya kati wanajiuliza, “Je, ujuzi wetu una thamani gani sokoni?”

Wengi hukosa fursa za kuendeleza ujuzi wao, na ndoto zao hufikia kizuizi cha ukosefu wa ajira.

Na kutokana na wingi wa vijana, sio wote wanaobahatika kwenda VETA. Miundombinu ya vyuo vya mafunzo haikidhi mahitaji ya kila mkoa au kijiji nchini, hali inayoongeza uhaba wa ajira na fursa. 

Kasi ya teknolojia na mapinduzi ya kidijiti inatoa fursa ya kuunganisha vijana wa kila kona ya Tanzania, kubadilisha ujuzi kuwa miradi halisi, na kuunda ajira kwa taifa zima.

Ni jukwaa la kidijitali  linalowezesha wahitimu wa VETA, vyuo vikuu, na wahitimu wa ufundi kushirikiana bila vizuizi vya kijiografia. 

Hii ni njia ya kuunganisha vijana, kuwawezesha kupata mafunzo ya kiteknolojia, mentorship, ushauri wa kifedha, na fursa za uwekezaji kupitia mfumo wa mtandaoni.

Jukwaa hili kila kijana anaweza kushiriki, vijana wanaweza kujiunga na moduli za mafunzo, kufanya majaribio ya miradi yao, na kushirikiana na wajasiriamali wengine, mentors, na wawekezaji.

Pia hub hii itaunganisha rasilimali kwa kusaidia kuunganisha wahitimu na mitandao ya biashara, uwekezaji na mashirika ya maendeleo, kuhakikisha miradi ya startups inaongezeka na kuunda ajira.

Na baada ya uanzishwaji wake sasa hatua ya mbeleni ni kutengeneza hubs kwa kila mkoa ili kuwezesha vitendo vya majaribio, kukuza biashara na upanuzi wa uwekezaji kwa vijana wa mikoa husika.

Tija yake ni kubwa mosi, inatoa uchechemuzi wa ajira kwa vijana wote, sababu sio kila kijana ana nafasi ya kuingia VETA au vyuo vya ufundi.

Hata hivyo, itawawezesha vijana kubadilisha maarifa yao kuwa startups, bidhaa, au huduma zinazouzwa sokoni.

Zaidi, itakuwa darasa huru kwa nchi nzima kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwa wajasiriamali wenye uzoefu na mentors wa kitaifa na kimataifa.

Aidha, kasi ya teknolojia na mapinduzi ya kidigitali itawawezesha kutumia mfumo wa mtandaoni kuunda miradi yenye thamani na kuvutia uwekezaji.

Inatoa jukwaa la kushirikiana kwa vijana kutoka kila kona ya nchi, kuondoa pengo la kijiografia na usawa wa fursa. 

Kwenye kampeni hizi wengi wanakosa kuzungumzia sera hii kwa kina jambo ambalo ni kasoro kubwa, kwani vijana ndio nguvu ya taifa na kundi kubwa la wapiga kura. 

Kupuuza ajenda ya Innovation Hubs ni kupuuza mustakabali wa ajira na maendeleo.

Ni wakati mwafaka wa kuanza kuunda taskforce ya kitaifa kwa ajili ya kuanza kuendesha pilot hub mtandaoni.

Hii itapendeza zaidi kwa kwenda sambamba na uanzishaji wa mfuko maalum wa programu 'seed fund,' ili kuweka wepesi wa kufanikisha majukumu yake.

Innovation Hubs siyo tu sera nzuri; ni njia thabiti ya kuunda ajira, ujasiriamali, uthubutu, kubadilisha mitazamo ya vijana na  maendeleo ya kweli.


 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad