MHE. MCHENGERWA ASHIRIKI SWALA YA EID EL FITRI KINONDONI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, March 22, 2026

MHE. MCHENGERWA ASHIRIKI SWALA YA EID EL FITRI KINONDONI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi wa Dini mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kushiriki swala ya Eid El-Fitri katika Msikiti Mkuu wa BAKWATA (Mfalme Mohamed VI), Kinondoni jijini Dar es Salaam Machi 21, 2026.
#Watanzania waaswa kulinda amani.

Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Machi 21, 2026  ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na waumini wa dini ya Kiislam kwenye  Swala ya Eid El-Fitri katika Msikiti Mkuu wa BAKWATA (Mfalme Mohamed VI), Kinondoni, jijini Dar es Salaam. 

 

Ibada hiyo ya kitaifa iliyoongozwa na Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Bin Zubeir, inayofanyika mara baada ya kumalizika  kwa siku 30 za mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan Machi 20, 2026

 

Pia ibada ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule.

 

Katika ibada hiyo Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Bin Zubeir, amehimiza amani, umoja na mshikamano kwa  waumini wa kiislam na watanzania kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad