Nilikuwa naamini ndoa yangu ilikuwa imesimama kwenye msingi wa kuaminiana. Mimi na mume wangu tulikuwa tumetoka mbali pamoja. Tulijenga maisha yetu hatua kwa hatua, tukapitia changamoto nyingi, na licha ya mabishano ya kawaida ya ndoa, nilikuwa naamini hakuna jambo ambalo lingeweza kututenganisha kirahisi.
Lakini ghafla mambo yakaanza kubadilika kwa namna ambayo sikuielewa. Mwanzoni ilikuwa ni vitu vidogo vidogo. Mume wangu alianza kubadilika taratibu. Simu yake ambayo zamani ilikuwa wazi kwangu ghafla ikaanza kuwa siri kubwa. Alianza kuiweka silent kila wakati.










No comments:
Post a Comment