Mtoto miaka 9 wa kituo cha watoto Yatima wenye Mahitaji Malum Kisweru Kilosa, aongoza Sala ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan baada kukabidhiwa zawadi ya Edi ( vyhakula na Ngo'mbe 3) vilivyotolewa na Mhe Rais
Awaliza viongozi na wazazi kwa namna walivyoguswa na kujawa na moyo wa Shukran katika maombi hayo.
Zawadi mbali mblali ikiwemo Vyakula (Mchele, Sukari, mafuta ya kula, Sabuni ya kufulia, Maharagwe) na Jumla ya Ngo'mbe 6,000 zimetolewa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassam kwa wananchi wa Wilaya ya Kilosa pamoja na makundi maalum katika kusherehekea sikukuu ya Edi Al Adhar zoezi lililongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Shaka Hamdu Shaka.










No comments:
Post a Comment