Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na  Wananchi wa Kijiji cha Mambegwa mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki wakati akisikiliza kero zao.

......................................

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

MKUU wa Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro  Shaka Hamdu Shaka amesema Serikali imepokea malalamiko na vilio vya wananchi kuhusu tukio lililotokea eneo hilo, huku akiahidi kuwa viongozi watarudi na majibu baada ya kufanya uchunguzi wa kina.

Akizungumza na Wanaaanchi wa Kijiji cha Mambegwa huku akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Shaka alisema wamezisikia sauti za kina mama, wazee na vijana na kuwataka kuwa na imani na viongozi wao.

“Tumekisikia kilio chenu kina mama, tumesikia sauti zenu vijana na wazee. Naomba mtuamini, tunaondoka na jambo hili kwa uzito mkubwa na tutarudi na majibu,” alisema.

DC Shaka alisema kwa sasa viongozi hawana majibu ya moja kwa moja kuhusu kilichotokea, lakini Serikali haiwezi kukwepa jukumu la kutafuta ukweli na ufumbuzi wa tatizo hilo kwa manufaa ya wananchi.

Mmoja wa Wananchi waa Kijiji cha Mambegwa akitoa kero kuhusu kijiji hicho.

Wananchi wa Kijiji cha Mambegwa wakiwa kwenye mkutano huo.