Kwa miaka mingi nilikuwa najituma sana kazini. Nilikuwa nafika mapema, kufanya kazi zangu kwa uaminifu, na kuhakikisha kila jukumu nililopewa linamalizika vizuri. Nilikuwa naamini siku moja juhudi zangu zingetambuliwa. Lakini kadri miaka ilivyopita, matumaini yangu yalianza kupungua.
Kilichoniumiza zaidi ni kuona watu waliokuja kazini baada yangu wakianza kupandishwa vyeo mmoja baada ya mwingine huku mimi nikibaki pale pale. Wengine walikuwa hata wananiuliza maswali ya kazi kwa sababu nilikuwa na experience zaidi yao lakini mwisho wa siku wao ndio walikuwa wanapewa nafasi nzuri.
Kwa kweli iliniuma sana.




0 Comments