Na.OWM (KAM),Songea
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuwekeza katika ukuzaji wa ujuzi kwa vijana kupitia Programu ya Taifa ya Uanagenzi inayotekelezwa katika vyuo mbalimbali nchini. Miongoni mwa vyuo vinavyonufaika na mpango huo ni Chuo cha Ufundi Peramiho kilichopo Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma.
Kupitia programu hiyo, serikali imefadhili mafunzo kwa vijana 125 katika chuo hicho chenye historia ya miaka 98 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1928 na wamisionari kutoka Ujerumani. Chuo hicho kimeendelea kuwa kitovu cha utoaji wa elimu ya ufundi na stadi za kazi kwa vijana wa Kitanzania.
Mkuu wa Chuo hicho, Fr. Martin Mrope, akizungumza na mwandishi wetu (04 Mei 2026) Peramiho alisema katika awamu ya nane ya programu hiyo 2025/206 jumla ya vijana 118 wanaendelea na mafunzo katika fani tano ambazo ni ubunifu wa mitindo na ushonaji, ufundi wa mabomba, useremala, ufundi magari na umeme wa majumbani.
Alisema mafunzo hayo ya miezi minane yanayofadhiliwa na Serikali upitia Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi,Ajira na Mahusiano yanajumuisha miezi sita ya nadharia na vitendo darasani pamoja na miezi miwili ya mafunzo kwa vitendo kazini. Lengo ni kuwajengea vijana uwezo wa kujitegemea, kuajiriwa au kujiajiri kupitia stadi wanazopata.
Baadhi ya wanagenzi wamesema tayari wameanza kupata uwezo wa kufanya kazi za ufundi hata kabla ya kuhitimu mafunzo yao. Kati yao Januari Mwakilambo anayesomea ufundi wa mabomba alisema sasa anaweza kuchora mifumo ya maji ndani ya nyumba huku Shakira Sinakara akieleza kuwa alichagua fani hiyo ili kusaidia upatikanaji wa huduma za mafundi vijijini.
Kwa upande wake, mwanagenzi wa fani ya umeme wa majumbani Ali Hamis Kaukuya alisema mbali na ujuzi wa kazi, mafunzo hayo yamewajengea maadili na uaminifu katika kazi za ufundi. Naye David Mapunda ameishukuru serikali kwa kugharimia mafunzo yanayowapa uhakika wa kupata ujuzi ndani ya muda mfupi.
Wakufunzi wa chuo hicho wameipongeza serikali kwa kuendelea kuwezesha vijana wengi kupata mafunzo ya ufundi ambapo Mkufunzi wa umeme, Sista Deogratia Mauki, alisema programu hiyo imeongeza ushiriki wa wasichana katika fani za ufundi na kuwasaidia kujitegemea kiuchumi.
Takwimu za serikali zinaonyesha kuwa vijana 5,746 wananufaika na programu hiyo katika vyuo 46 nchini kwa mwaka 2025/26. Serikali pia imetenga shilingi bilioni moja katika bajeti ya mwaka 2026/27 kusaidia wahitimu wa mafunzo ya uanagenzi kupata vitendea kazi kwa ajili ya kujiajiri mara baada ya kuhitimu mafunzo haya ya muda mfupi.

0 Comments