𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐃𝐀 𝐒𝐄𝐍𝐆𝐀 𝐀𝐒𝐇𝐔𝐊𝐔𝐑𝐔 𝐔𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐊𝐀 𝐌𝐒𝐈𝐁𝐀 𝐖𝐀 𝐄𝐗-𝐒𝐀𝐉𝐄𝐍𝐓𝐈 𝐘𝐄𝐒𝐀𝐘𝐀 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Monday, June 22, 2026

𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐃𝐀 𝐒𝐄𝐍𝐆𝐀 𝐀𝐒𝐇𝐔𝐊𝐔𝐑𝐔 𝐔𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐊𝐀 𝐌𝐒𝐈𝐁𝐀 𝐖𝐀 𝐄𝐗-𝐒𝐀𝐉𝐄𝐍𝐓𝐈 𝐘𝐄𝐒𝐀𝐘𝐀

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga, amewaongoza Maafisa, Wakaguzi, Askari wa vyeo mbalimbali pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Songwe katika shughuli ya kumuaga Ex-Sajenti Yesaya Ifuja aliekuwa anafanya kazi Wilaya ya Mbozi, ambaye alikuwa mume wa Sajenti Felister Nawe, aliefariki Juni 20, 2026 katika Hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya kuugua.


Akizungumza Juni 21, 2026 wakati wa kuaga mwili wa marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea Mji wa Kateshi, Wilaya ya Hanang, Mkoani Manyara kwa ajili ya mazishi, Kamanda Senga amewashukuru wananchi waliojitokeza kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe katika masuala ya usalama na kijamii, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza mshikamano katika masuala ya kijamii bila kujali nafasi au majukumu ya mtu katika jamii.


Katika hatua nyingine, Kamanda Senga amewashukuru viongozi wa Serikali na wa dini, ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wote waliojitokeza kushiriki katika shughuli ya kumuaga marehemu na akiwaomba wananchi hao kuendelea na ushirikiano huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad