Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la taaluma la Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, Juni 27, 2026.
Kulia kwake ni Naibu Waziri Wizara ya Fedha, Mhandisi Mshamu Ali Munde na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata.
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akifurahia baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la taaluma la Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida Juni 27, 2026.
Wengine kutoka kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga, Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata na wa tano kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Mhadisi Mshamu Ali Munde.
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la taaluma la Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida ambalo Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba aliweka jiwe la msingi la ujenzi wake, Juni 27, 2026.
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na Naibu Waziri wa Fedha, Mhandisi Mshamu Ali Munde (kushoto) na Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Profesa William Pallanyo baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la taaluma la Taaisisi ya Uhasibu Tanzania Kampasi ya Singida, Juni 27, 2026.
Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na viongozi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) baada ya kuweka jiwe la Msingi Jengo la Taaluma, katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, lililokamilika kwa asilimia 63.
Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akipokea taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Prof. Jehovaness Aikael, baada ya kuweka jiwe la Msingi Jengo la Taaluma, katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, lililokamilika kwa asilimia 63, katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya TIA, Prof. William Pallangyo.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Prof. Jehovaness Aikael na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya TIA, Prof. William Pallangyo kabla ya kuwekwa jiwe la Msingi Jengo la Taaluma, katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, lililokamilika kwa asilimia 63.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo, kukagua Jengo la Taaluma la Taasisi hiyo lililokamilika kwa asilimia 63, kabla ya kuwekwa jiwe la msingi na Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.
Waziri Mkuu, Dkt, Mwigulu Nchemba akifurahia burudani ya ngoma baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, Juni 27, 2026.
Kushoto kwake ni Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Profesa William Pallangyo
Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), pamoja na Viongozi wa Mkoa na baadhi ya Wajumbe kutoka Wizara ya Fedha baada ya kuwekwa jiwe la Msingi Jengo la Taaluma, katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, lililokamilika kwa asilimia 63
Waziri Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na Wanachuo wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la taaluma chuoni hapo.
NA MPIGA PICHA WETU. SINGIDANI BLOG
















No comments:
Post a Comment