𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀𝐌𝐄𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐊𝐔𝐍𝐔𝐅𝐀𝐈𝐊𝐀 𝐍𝐀 𝐇𝐔𝐃𝐔𝐌𝐀 𝐙𝐀 𝐀𝐅𝐘𝐀 𝐇𝐎𝐒𝐏𝐈𝐓𝐀𝐋𝐈 𝐘𝐀 𝐁𝐄𝐍𝐉𝐀𝐌𝐈𝐍 𝐌𝐊𝐀𝐏𝐀 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, June 18, 2026

𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀𝐌𝐄𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐊𝐔𝐍𝐔𝐅𝐀𝐈𝐊𝐀 𝐍𝐀 𝐇𝐔𝐃𝐔𝐌𝐀 𝐙𝐀 𝐀𝐅𝐘𝐀 𝐇𝐎𝐒𝐏𝐈𝐓𝐀𝐋𝐈 𝐘𝐀 𝐁𝐄𝐍𝐉𝐀𝐌𝐈𝐍 𝐌𝐊𝐀𝐏𝐀

DODOMA – JUNI 17, 2026

Wananchi mbalimbali wameendelea kutembelea banda la Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) lililopo katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma kwenye maonesho ya wiki ya utumishi wa umma na kunufaika na huduma za uchunguzi wa magonjwa ya macho, magonjwa ya ndani na mengine yasiyo ya kuambukizwa.


Aidha wananchi pia wamepatiwa huduma ya Elimu na ushauri wa kitaalamu wa Afya na namna bora ya kujikinga na kudhibiti magonjwa yakiwemo yasiyo ya kuambukiza ambayo yanasababisha madhara mengi ikiwemo idadi kubwa ya vifo.

Daktari wa Macho kutoka BMH Yohana Raphael amesema mwamko mkubwa wananchi wameonesha kwenye eneo la kuchunguza magonjwa ya macho.


“Wananchi idadi kubwa wamepata fursa ya kupata vipimo na elimu ya Afya ya macho ikiwemo magonjwa ya presha ya macho, mtoto wa jicho na Uvimbe wa macho” alisisitiza Dkt. Raphael.


Akitoa maoni yake baada ya kutembelea banda la BMH Mwananchi Alex Muhulo amesema kuwa ni vizuri kupima Afya mara kwa mara ili kuweza kutambua hali yako ya kiafya, kujua mapema hali ya kiafya inasaidia kuchukua hatua za mapema za kulinda Afya yako, unaweza kupunguza changamoto zinazoweza kutokea endapo itagundulika una matatizo ya kiafya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad