𝐎𝐖𝐌 𝐘𝐀𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈 𝐌𝐀𝐎𝐍𝐄𝐒𝐇𝐎 𝐘𝐀 𝐖𝐈𝐊𝐈 𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐔𝐌𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐔𝐌𝐌𝐀 𝟐𝟎𝟐𝟔 𝐃𝐎𝐃𝐎𝐌𝐀 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, June 18, 2026

𝐎𝐖𝐌 𝐘𝐀𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈 𝐌𝐀𝐎𝐍𝐄𝐒𝐇𝐎 𝐘𝐀 𝐖𝐈𝐊𝐈 𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐔𝐌𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐔𝐌𝐌𝐀 𝟐𝟎𝟐𝟔 𝐃𝐎𝐃𝐎𝐌𝐀

Na, Mwandishi wetu – Dodoma

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Bi. Stella Mwaiswaga pamoja na Watumishi wengine kutoka Ofisi hiyo wameshiriki ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi tarehe 17 Juni, 2026 katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma. 


Maonesho ya Wiki ya Utumishi ni moja ya matukio katika kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchi wanachama huadhimisha kwa kaulimbiu moja na kufanya maonesho ya kazi mbalimbali kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma ambapo hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni. 


Kwa mwaka huu Maadhimisho hayo yamebeba kaulimbiu isemayo; *“Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi wa Huduma Endelevu”.*


SAmbamba na hilo Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu inashiriki maonesho hayo huku ikitoa elimu mbalimbali kwa umma kuhusiana na shughuli za Wakala Serikali wa uchapishaji Tanzania, elimu kuhusu masuala ya Menejimenti ya Maafa, Watu wenye Ulemavu, Ufuatiliaji na Tathimini pamoja na Masuala ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad