Mchungaji Dr. Lucas Dobogo
...............................
Kanisa la
Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Kigogo Kati Jijini Dar es
Salaam limeandaa mkutano mkubwa wa injili wa siku saba za wokovu, uponyaji naa
kufunguliwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mchungaji mwenyeji wa mkutano huo, Dr. Lucas Dobogo
alisema mkutano huo utaanza Juni 22, 2026 na utafikia tamati Juni 28, 2026.
“Mkutano huo
utafanyika Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Kigogo
Kati Jijini Dar es Salaam kuanzia Saa 9 alasiri
kila siku watu wote wanakaribishwa,” alisema Mchungaji Dobogo.
Alisema
katika mkutano huo Kwaya ya Victory ambayo itakuwa mwenyeji na Kwaya ya Palanjo
Family kutoka Arusha zitahudumu.
Aidha,
Mchungaji Dobogo alisema kwenye mkutano huo wagonjwa, watu wenye shida
mbalimbali wataombewa bure na amewataja Wachungaji watakao hubiri kuwa ni
Joseph Ndaki, Keneth Mazengo na Dr. Lucas Dobogo.
Kwa
mawasiliano zaidi kuhusu mkutano huo unaweza kupiga namba 0658972055 na
0686815230.
......................
Habari hii imeandikwa na Dotto Mwaibale Simu namba 0754-362990









No comments:
Post a Comment