Kujitoa mhanga kwa miaka mingi kuwasomesha watoto, kuwauguza, na kujinyima kila kitu ili wapate maisha mazuri ni jukumu ambalo kila mzazi analibeba kwa upendo na matumaini ya kutunzwa uzeeni.
Hata hivyo, pale watoto hao wanapofanikiwa, wakapata kazi nzuri na maisha ya kifahari mjinikisha wakakusahau kabisa na kukutelekeza kwenye uzee wako, maumivu yake ni makali mno kuliko ugonjwa wowote.
Nilipambana sana kulea watoto wangu watatu baada ya kufiwa na mume wangu; niliuza shamba na kukopa ili kuhakikisha wote wanahitimu elimu ya chuo kikuu. Cha kusikitisha, baada ya kupata kazi zenye mishahara mikubwa, walibadilika kabisa.










No comments:
Post a Comment