𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀 𝐔𝐙𝐈𝐍𝐃𝐔𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐙𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄𝐊𝐈𝐓𝐈 𝐂𝐂𝐌 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐓𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐀𝐌𝐁𝐎 𝐁𝐀𝐌𝐔 𝐁𝐀𝐌𝐔 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, September 19, 2026

𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀 𝐔𝐙𝐈𝐍𝐃𝐔𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐙𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄𝐊𝐈𝐓𝐈 𝐂𝐂𝐌 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐓𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐀𝐌𝐁𝐎 𝐁𝐀𝐌𝐔 𝐁𝐀𝐌𝐔

Kuzinduliwa leo Wilaya ya Panga

Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM wa Wilaya ya Pangani, Ramadhani Seif,  (Mabuyu), akizungumza wakati wa uhamasishaji wa matukio mbalimbali kabla ya kufanyika uzinduzi huo Septemba 19, 2026 Kijiji cha Stahabu Azimio.

.....................

MKUTANO wa Hadhara wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kwa ajili ya kuzinduliwa  rasmi ziara za Mwenyekiti wa CCM mkoa huo  na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Ustadhi Rajabu Abdalrahaman  unafanyika leo Septemba 19, 2026 Kata ya Mikunguni, Kijiji cha Stahabu Azimio, Wilaya ya Pangani. 


Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM, Wilaya ya Pangani, Ramadhani Seif (Mabuyu) amesema awali ya yote watawapokea wageni kutoka sehemu mbalimbali ya Mkoa wa Tanga na kisha viongozi wa ngazi ya mkoa akiwepo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga.


Alisema baada ya mapokezi hayo zitafanyika burudani mbalimbali.


“Baada ya utambulisho wa wilaya itafuata itifaki ngazi ya mkoa ikiongonzwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo Mkoa wa Tanga, Samuel Ngazija,”

 

alisema, Seif (Mabuyu)

Katika mkutano huu wananchi wengi wamefika kusikia mambo mbalimbali yatakayo zungumzwa na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Tanga huku rangi ya kijani ikiwa imekifunika Kijiji cha Stahabu kilichopo Kata ya Mikunguni.


Baadhi ya viongozi ambao wamehudhuria mkutano huo ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Wajumbe wa kamati za siasa Mkoa na Wilaya, viongozi wa jumuiya zote za CCM Mkoa wa Tanga, Madiwani, viongozi wa dini, Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Gilbert Kalima ambaaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa  na baadhi ya wasanii kutoka Unguja wakiungana na wa Mkoa wa Tanga kama vile Seku Segumbo na Zanzibar, Haitham Khamis Hassan na Asha Amie ambao wanaimba utenzi..


Baada ya uzinduzi huo ziara hiyo itaendelea kesho Wilaya ya Handeni na Septemba 25-26, 2026 watampokea Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongozi ambaye atakuwa mkoani hapa kwa ziara ya kikazi.Wana CCM wakiwa kwenye mkutano.Wanawake wa CCM wakiwasili Viwanja vya Stahaabu Azimio kwa ajili ya mkutano huo.

Wanawake wa CCM wakisubiri kuanza kwa mkutano huo.Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa waa Tanga, Lucy Benjamini, Doris Moshi, Asha  Ruso Kada wa chama hicho, Zena Ruge na Wasanii wa Utenzi kutoka Unguja Zanzibar Haitham Khamis (wa pili kulia) na  na Asha Amie (kulia)
Wasanii kutoka Zanzibar, Haitham Khamis Hassan (kushoto) na Asha Amie wakiwa kwenye uzinduzi huo kabla ya kuanza.
Wananchi wakiwa kwenye mkutaano huo.
Wananchi na Wana CCM wakisubiri kuanza kwa uzinduzi huo.
Gari maalumu lililonunuliwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga kwa ajili ya matangazo ya mikutano mbalimbali mkoani Tanga likitumika kutoa matangazo kwenye uzinduzi huo..
Makada Kindakindaki wa CCM Mkoa waa Tanga wakiwa kwenye uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Ibrahim Kizulwa, Haji Machaku, Nurdin Abubakari, Ally Umudi naa Hamadi Hamisi.
Makada wa CCM wa Tanga wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Makada Kindakindaki wa CCM wakiwa kwenye mkutaano huo kabla ya kuanza kwa uzinduzi huo.
............................................

Habari hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad