Jina langu ni Baraka. Kubambikiwa kesi ya uongo na kutishiwa kifungo cha jela kwa kosa usilolijua ni mateso makubwa yanayoweza kukunyang’anya amani, heshima, na kuitumbukiza familia yako kwenye simanzi nzito.
Kwa miezi kadhaa, nilikuwa nikipitia kipindi kigumu zaidi maishani mwangu baada ya baadhi ya maadui na washindani wangu wa kibiashara kunisuka njama mbaya na kunibambikia kesi nzito ya jinai polisi.
Walipanga mashahidi wa uongo, wakatengeneza ushahidi wa kughushi, na kuhakikisha kesi hiyo inafika mahakamani ikiwa na shinikizo kubwa la kunifunga mimi miaka mingi jela ili wachukue biashara na mali zangu.










No comments:
Post a Comment