Gharama za kuingia kwenye kinyang’anyiro cha uongozi na kisiasa ni kubwa, lakini uchungu mkubwa zaidi ni pale unapoona juhudi, rasilimali, na nia yako njema kwa wananchi zikizikwa na mawimbi ya chuki, matope, na ushirikina kutoka kwa wapinzani wako.
Miezi michache kabla ya uchaguzi, nilikuwa miongoni mwa wagombea waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda.
Hata hivyo, mara tu kampeni zilipopamba moto, upepo ulibadilika ghafla wapinzani wangu walisuka njama nzito za kunitengenezea skandali za uongo, kunipaka matope kwenye mikutano ya hadhara, na kuniharibia jina kabisa mbele ya mpiga kura.
Kila nilipojaribu kusimama jukwaani kuhutubia, wananchi walikuwa wakinionyesha dharau, kunizomea, na kukataa kusikiliza sera zangu. Nilibaki nikitazama ndoto yangu ya uongozi na mamilioni ya fedha nilizowekeza zikitumbukia nyongo.










No comments:
Post a Comment