TANESCO SINGIDA YAHIMIZWA KUTOA HUDUMA BORA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Wednesday, October 7, 2026

TANESCO SINGIDA YAHIMIZWA KUTOA HUDUMA BORA


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Joanfaith Kataraia, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Singida, Gondwin Gondwe, akizungumza wakati akifungua kikao cha TANESCO na wateja wakubwa wa umeme kilichofanyika Oktoba 7, 2026.
---------------------------
👇ANGALIA VIDEO HAPA

 

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida limetakiwa kuendelea kutoa huduma bora, za uhakika na zinazozingatia mahitaji ya wateja. 


Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Joanfaith Kataraia, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Singida, wakati akifungua kikao cha TANESCO na wateja wakubwa wa umeme kilichofanyika Oktoba 7, 2026. 


Kataraia alisema kikao hicho ni fursa muhimu ya kuimarisha ushirikiano kati ya TANESCO na wateja wake wakubwa, kusikiliza maoni yao, kujadili changamoto na kutafuta suluhisho kwa pamoja. 


“Napenda kuwapongeza TANESCO kwa kuandaa kikao hiki muhimu katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. Kikao hiki ni fursa muhimu ya kuimarisha ushirikiano kati ya TANESCO na wateja wake wakubwa,” alisema Kataraia. 

 

Alisema umeme ni nguzo muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, huku akieleza kuwa wateja wakubwa, hususan katika sekta ya viwanda, biashara na taasisi mbalimbali, wanategemea huduma hiyo ili kuongeza uzalishaji na kuchangia maendeleo ya Mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla. 


Aidha, aliwahimiza wananchi na wateja wa TANESCO kuendelea kushirikiana na shirika hilo kwa kulipa ankara kwa wakati, kutoa taarifa za changamoto mapema na kutumia nishati kwa ufanisi. 


Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Ben Kirumba, aliwashukuru wateja wakubwa kwa ushirikiano wao na shirika hilo, akisema mchango wao ni muhimu katika kuendelea kulifanya shirika liendelee. 


Kirumba alisema kukamilika kwa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere na kuanza kuingiza umeme kwenye Gridi ya Taifa ni hatua kubwa ambayo inapaswa kuendana na matumizi makubwa ya umeme katika shughuli za uzalishaji na maendeleo. 


“Umeme unaozalishwa unatakiwa kutumika na wadau wetu ambao ndio wanaoutumia kwa shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi,” alisema. 

 

Alisema kupitia Kurugenzi ya Huduma kwa Wateja, TANESCO imeendelea kufanya maboresho mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kusogeza huduma karibu na wateja. 


Alisema maboresho hayo yanaendana na kaulimbiu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja inayosema “Extra Mile”, yenye lengo la kusogeza huduma karibu, kuongeza uaminifu na kulinda uzalishaji wa mteja. 


Naye Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Singida, Rehema Mwaipopo, alisema matumizi ya juu ya umeme katika Mkoa wa Singida kwa sasa yanafikia megawati 30.578. 


Alisema hali hiyo inaonyesha kuwa mkoa huo bado una nafasi kubwa ya kuvutia wawekezaji, hususan katika sekta ya viwanda. 


“Hii inatuambia nini? Mkoa wetu wa Singida bado unahitaji wawekezaji wa viwanda kwa kiasi kikubwa kwa sababu tumepata neema ya kuwa katikati ya Tanzania. Kituo chetu kimekuwa kikubwa na kuwekewa uwezo mwingi, lakini matumizi yake ni machache sana,” alisema Mwaipopo. 

 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa  wa Chemba ya Wafanyabiashara Mkoa wa Singida (Tanzania National Chamber of Commerce – TNCC), Kitila Katala, aliishukuru TANESCO kwa maboresho mbalimbali iliyoyafanya katika utoaji wa huduma. 


Alisema wafanyabiashara, ambao ni injini ya uchumi wa nchi kupitia sekta binafsi, wana mchango mkubwa katika kufanikisha dira ya maendeleo ya Taifa ya 2050. 


Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya SUMACO Engenering Ltd, Fenny Mashara, aliipongeza TANESCO kwa maboresho makubwa iliyoyafanya katika utoaji wa huduma kwa wateja.

Kaimu Meneja wa Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Ben Kirumba, akizungumza katika kikao hicho.
Mhandisi wa Shirika hilo Mkoa wa Singida, Boniface Shitindi akijibu maswali ya wateja.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Singida, Rehema Mwaipopo, akizungumzia masuala mbalimbali yanayohusu uzalishaji wa umeme.
Selemani Nkuna kutokaa Kampuni ya Shenda Limited akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Albert  Theonas Mathias kutoka RUWSA- Manyoni akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi wa Lombearuke Ranko Blandi (maarufu Mnaigeria), akichangia jambo.
Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (RUWASA)< Wilaya ya Manyoni- Itigi, Mhandisi Lucas Mwinuka, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Juventus Charles kutoka Hospitali ya St. Gasper Itigi akichangia jambo kwenye kikao hicho
Mzee Iddi Swalehe Mwanja akiuliza swali.
General Manager (Rift Valley Concret Works), Chris Konga, akitambulisha kampuni yake na kuchangia baadhi ya mambo.
Mwenyekiti wa  wa Chemba ya Wafanyabiashara Mkoa wa Singida (Tanzania National Chamber of Commerce – TNCC), Kitila Katala, akichangia jambo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya SUMACO Engenering Ltd, Fenny Mashara, akiipongeza Tanesco kwa maboresho.
Meneja wa Taanesco Wilaya ya Mkalama, akitoa neno la shukrani.
Wadau wa Tanesco wakiwa kwenye maadhimisho hayo
Wadau wa Tanesco wakiwa kwenye kikao hicho.



Viongozi wa Tanesco Mkoa wa Singida wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Kikao kikiendelea
Maadhimisho yakiendelea.
Afisa Rasilimali Watu Tanesco, Singida Angelina Karata (kulia) na Mwandishi Mwendesha Ofisi Ikungi, Yusra Nikolaus wakiwa katika ubora wao kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Joanfaith Kataraia, akikabidhiwa jiko la umeme.
Vyeti vikikabidhiwa
Vyeti vikikabidhiwa kwa Wateja wa shirika hilo.
Tuzo Maalumu waliyotunukiwa Tanesco Singida katika Maadhimisho ya mwaka 2025 wakikabidhiwa na Kaimu Meneja wa Huduma kwa Wateja wa shirika hilo, Ben Kirumba (kulia).
Wateja Wakubwa wa Tanesco wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi wa shirika hilo baada ya kutunukiwa vyeti. Wateja hao ni Erneus Mwemezi kutoka Kampuni ya Shanta Mine (waliosimama kulia), Novin Staanslaus kutoka Kampuni ya Mount Meru (katikati) na Manager wa Trible SevenMining Ltd. .
Muonekano wa Keki Maalumu ya Maadhimisho hayo
Keki Maalumu ya Maadhimisho hayo ikikatwa.
Meneja waa Tanesco Wilaya yaa Mkalama, akiwapa keki wafanyakazi wenzake.
Picha ya pamoja.
Wafanyakazi wa Tanesco wakiwa katika pichha ya pamoja.
Wadau wa Tanesco wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Tanesco.
---------------------
Imeandaliwa na Mtandao wa Singidani Blog.

0754362990 / 0787 013 988

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad