KUELEKEA MICHUANO YA AFCON, DKT. KIJAJI AWAKARIBISHA WANASOKA TANZANIA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Wednesday, November 25, 2026

KUELEKEA MICHUANO YA AFCON, DKT. KIJAJI AWAKARIBISHA WANASOKA TANZANIA

Nyumbani ni nyumbani. Huo ndio ujumbe wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alioutoa Novemba 25, 2026 alipowaalika wapenda soka kutoka maeneo mbalimbali duniani kuitembelea Tanzania kushuhudia mashindano ya AFCON na kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Akizungumza katika tukio maalum la kusaini mkataba wa haki za urushaji wa matangazo ya AFCON, ambazo Tanzania imezipata kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Dkt. Kijaji amesema kuwa vivutio vya utalii vilivyopo nchini pamoja na mashindano ya soka vitawapa wageni fursa ya kufurahia kipindi chote cha michuano hiyo.

“Wanasoka, karibuni nyumbani Tanzania, sehemu pekee yenye vivutio vya utalii vya kipekee, kuanzia historia ya binadamu wa kale iliyopo Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro, Serengeti na fukwe za kupendeza za Zanzibar,” alisema Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kushirikiana na Marais wengine wa Afrika Mashariki katika kufanya maamuzi ya mashindano hayo kufanyika katika nchi hizo, akisema hatua hiyo itafungua fursa katika sekta ya utalii na mnyororo wake wa thamani.

Ngorongoro inatajwa kuwa eneo lenye ushahidi wa kisayansi wa nyayo za binadamu wa kale waliotembea kwa miguu miwili katika eneo la Laetoli, historia inayolifanya eneo hilo kuwa miongoni mwa vivutio muhimu vya urithi wa binadamu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad