Ilikuwa saa sita usiku niliposhtuka kutoka usingizini bila sababu ya kueleweka. Nilihisi kitu si cha kawaida ndani ya nyumba yangu. Mume wangu hakuwa kitandani, jambo ambalo halikuwa la kawaida kabisa. Nilinyanyuka kimya kimya na kuanza kumtafuta.
Nilipofika sebuleni, nilisikia sauti za chini chini. Moyo wangu ulianza kudunda kwa kasi. Niliposogea karibu, nilichokiona kiliniacha bila pumzi. Mume wangu alikuwa akiongea kwa siri na mwanamke mwingine kupitia simu, na maneno yao yalikuwa ya kimapenzi waziwazi. Nilihisi kusalitiwa na kudharauliwa.










No comments:
Post a Comment