Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya kuwa Kinara wa
Dhana ya Urekebishaji wa Wafungwa Magerezani kutoka kwa Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi Mhe. Patrobas Paschal Katambi pamoja na Kamishna Jenerali wa
Magereza Jeremia Yoram Katungu kwenye hafla ya hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya
Uongozi Ngazi ya Juu Kozi namba 28 na Uongozi Daraja la Pili Kozi namba 48 ya
mwaka 2025/2026 katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga
Jijini Dar es Salaam Mei 9, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha tuzo hiyo...........................................
KWA mara ya
kwanza tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Magereza Tanzania, mkuu wa nchi, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Tuzo Maalumu
ya Kinara wa Dhana ya Urekebishaji wa Wafungwa Magerezani (Champion of Prisoner
Rehabilitation Concept Award) hatua inayotajwa kuwa ishara ya mageuzi makubwa
ya kifalsafa, kiutendaji na kimaendeleo ndani ya mfumo wa haki jinai nchini.
Tuzo hiyo
aliyokabidhiwa Rais Samia, Mei 9, 2026 katika Chuo cha Taaluma ya
Urekebishaji Tanzania haionekani tu kama pongezi kwa uongozi wa Serikali, bali
kama alama ya mabadiliko ya kihistoria yanayoibadilisha falsafa ya magereza kutoka
mfumo wa adhabu kwenda mfumo wa urekebishaji, elimu na maendeleo ya binadamu.
Mageuzi hayo yanasimamiwa kwa karibu na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, CGP Jeremiah Yoram Katungu, ambaye chini ya uongozi wake jeshi hilo limeendelea kufanya maboresho makubwa ya kiutendaji, matumizi ya teknolojia na utoaji wa mafunzo ya kisasa ya urekebishaji.
KUENDELEA KUSOMA MAKALA HII










No comments:
Post a Comment