.......................................
Na Onesmo Kapinga
UONGOZI wa Kanisa la Jesus Power Revival Center (RC), umeandaa kongamano kubwa la kimataifa kwa lengo la kuelimisha na kuwapa ujumbe watumishi wa Mungu na kanisa kwa ujumla.
Kongamano hilo, litafanyika kwa siku tano kuanzia Septemba 2, mwaka huu, katika Makao Makuu ya Kanisa la RC yaliyopo Pugu Stesheni, Ilala jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia kongamano hilo, Askofu Prince Emmanuel Chomba, alisema maaskofu na wahubiri mbalimbali wanatarajiwa kuja nchini kuhubiri katika kongamano lao, ambalo litakuwa la kihistoria.
Askofu Chomba alisema katika kongamano hilo, kutakuwapo wahubiri kutoka Marekani, Kenya, Uganda, Msumbiji, Malawi, Zambia, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Alisema kwanya za injili kutoka nchi mbalimbali zimealikwa kwa ajili ya kuenjilisha katika kongamano hilo kubwa ambalo halijawahi kufanyika kanisani hapo.
Askofu Chomba alisema makanisa yote ya Pentekoste ya Ilala yatashiriki kongamano litakalofanyika kwa siku tano.
"Watu wa Mungu wataelimishwa katika dhama hizi za mwisho za ujio wa Yesu," alisema Askofu Chomba.
Pia Askofu Chomba alisema katika dhama hizi waumini wataelimisha dhama za sasa, kwani dunia inapobadilika na kanisa linahitaji kubadilika tofauti na zamani.
Askofu huyo, alisema dhama za sasa neno la Mungu linahubiriwa kwa kutumia vyombo vya muziki ili kuwafikia watu wengi tofauti na zamani.
Alisema kwa kuwa dunia inaenda kasi, kama watu hawataelimishwa maasi yataongezeka, hivyo kongamano hilo litakwenda kuelimisha jamii na washirika wao.
Mtumishi huyo wa Mungu alisema watoto wadogo wanashinda mitandaoni na wale wa kike vigodoro kama kanisa linajukumu la kuielimisha jamii na jamii kuelimika.










No comments:
Post a Comment