Jina langu ni Daniel. Kufungua biashara kwa matumaini makubwa, kuweka bidhaa nzuri madukani, halafu kukaa siku nzima bila kuona sura ya mteja hata mmoja ni moja ya mateso makubwa yanayoweza kumfanya mfanyabiashara yeyote apate msongo wa mawazo na kukata tamaa.
Kwa miezi kadhaa, duka langu la vifaa vya ujenzi lilikuwa linapitia kipindi kigumu sana. Licha ya kuwa na bidhaa bora na bei nafuu ukilinganishwa na wengine, wateja walikuwa wanapita tu nje ya duka langu na kwenda kununua kwenye maduka mengine ya mbali.
Kila wiki nilikuwa najikuta nikiingia hasara ya kulipia pango la duka na kuacha mikopo ikiniongezea mzigo mkubwa, huku nikiwa sijui hatima ya maisha yangu na familia yangu.










No comments:
Post a Comment